9.3 C
New York

Staa mpya Liverpool abeba tuzo Ujerumani

Published:

MUNICH, Ujerumani
MSHAMBULIAJI mpya wa Liverpool, Florian Wirtz, ametwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa Ujerumani.
Wirtz aliyetua Anfield kwa ada ya Pauni milioni 116, amebeba tuzo hiyo kutokana na kiwango bora alichokuwa nacho msimu uliopita akiwa na Bayern Leverkusen.
Msimu uliopita, nyota huyo aliyewapiku Michael Olise, Nick Woltemade, Thomas Muller, aliifungia Leverkusen jumla ya mabao 16, pia akichangia ‘asisti’ 15.
“Katika soka, tuzo na mafanikio binafsi ni kitu kikubwa zaidi. Najua nina kazi kubwa ya kufanya kufikia ndoto za kuendelea kubeba tuzo za aina hii,” alisema Wirtz.
Kwa upande mwingine wa tuzo hizo, Julian Schuster wa Freiburg ndiye aliyeibuka kidedea katika kinyang’anyiro cha Kocha Bora wa Mwaka.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img