ISTANBUL, Uturuki
VIGOGO wa Ligi Kuu ya Uturuki, Besiktas, wamethibitisha kuinasa saini ya kiungo wa kimataifa wa Nigeria, Wilfred Ndidi.
Ndindi aliyeitumikia Leicester kwa miaka nane, amesaini miaka mitatu kuitumikia miamba hiyo akitokea Leicester City ya England.
Katika mkataba wake na Besiktas, kuna kipengele kinachoiruhusu klabu hiyo kumuongeza miezi 12 endapo itavutiwa na kiwango chake.
Taarifa zaidi zinaeleza kuwa Leicester wamevuna kitita cha euro milioni nane katika dili hilo.
Usajili huo unamfanya Ndidi aungane na Mnigeria mwenzake, Victor Osimhen, ambaye naye anakipiga Uturuki katika klabu ya Galatasaray.
Baada ya kuhusishwa na klabu kubwa nyingi za Ulaya, Osimhen alichagua kujiunga na Galatasaray akitokea Napoli, dili hilo likigharimu kitita cha euro milioni 75.
Published:


