MUNICH, Ujerumani
KLABU ya Bayern Munich imesitisha mkataba wa kuitangaza sekta ya utalii ya Rwanda kupitia ujumbe wa ‘Visit Rwanda’ kwenye jezi zake.
Hatua hiyo ya mabosi wa Bayern imetokana na kelele za muda mrefu za mashabiki wa klabu hiyo ya Bundesliga.
Februari, mwaka huu, mashabiki waliandamana wakiwa na mabango yenye jumbe za kulaani ushirikiano wao na Rwanda.
Kwa mashabiki wa Bayern, Rwanda imekuwa ikiwaunga mkono waasi wa M23 wanaoipa wakati mgumu Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).
Hata hivyo, licha ya kutangaza kuachana na ujumbe wa Visit Rwanda katika jezi, bado Bayern itaendeleza miradi ya kuibua vipaji kupitia ‘academy’ yao nchini Rwanda.
Lakini, bado ujumbe huo utaendelea kusomeka katika jezi za PSG, Arsenal na Atletico Madrid, ambazo hazijatangaza kufuata hatua hiyo ya Bayern.
Published:


