15 C
New York

Thomas Muller; miaka 15 ya mabao, ‘asisti’, rekodi Bayern

Published:

MUNICH, Ujerumani
JINA la Thomas Muller limetua Ligi Kuu ya Marekani (MLS) baada ya mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani kujiunga na Vancouver Whitecaps akitokea Bayern Munich.
Muller ameondoka Bayern akiwa ameifungia jumla ya mabao 250 kwa miaka zaidi ya 15 aliyoitumikia klabu hiyo ya mjini Munich. Ni tangu alipocheza mechi yake ya kwanza akiwa na umri wa miaka 19 mwaka 2008.
Kama hiyo haitoshi, Muller ameipa kisogo Bayern akiwa ndiye mchezaji aliyecheza mechi nyingi zaidi (756) katika historia ya klabu hiyo.
Akiwa Bayern, Muller aliwahi kufanya kazi na makocha mbalimbali, akiwamo Pep Guardiola. Wawili hao walifanya kazi pamoja kuanzia mwaka 2013 hadi 2016.
Kwa miaka mitatu waliyokuwa pamoja, Muller alifunga jumla ya mabao 79. “Ni mchezaji mwenye matumizi makubwa ya akili, asiyetabirika na anayejua cha kufanya,” anasema Guardiola akimzungumzia Muller.
Kwa upande mwingine, Muller akiwa na mabao 57, anashika nafasi ya tano katika orodha ya wafungaji bora wa muda wote wa Ligi ya michuano ya Mabingwa Ulaya.
Ikumbukwe, Muller ndiye aliyetwaa kiatu cha ufungaji bora wa fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2010 baada ya kuzifumania nyavu mara tano na kutoa ‘asisti’ tatu.
Mtandao wa OptaStats unaweka wazi kuwa tangu msimu wa 2008-09, hakuna mchezaji yeyote katika Ligi Kuu tano za Ulaya (England, La Liga, Bundesliga, Ligue 1 na Serie A) aliyemzidi Muller kwa asisti.
Mkurugenzi wa Bayern, Max Eberl, ameeleza ilivyokuwa ngumu kwake kutokumpa mkataba mpya mshambuliaji huyo. Eberl anasema alikosa usingizi kwa siku tatu baada ya kuona Muller akigomea mkataba mpya.
“Hakuna maneno yanayotosha kumsifia Muller,” alisema Eberl, ambaye aliajiriwa na Bayern mwaka jana.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img