MERSYSIDE, England
BAADA ya kumalizana na Al-Hilal, Darwin Nunez atavuna mshahara wa Pauni milioni 20 (takriani Sh bil. 68 za Tanzania) kwa mwaka kutoka kwa klabu hiyo ya Ligi Kuu ya Saudi Arabia.
Nunez, raia wa Uruguay mwenye umri wa miaka 26, anaelekea Uarabuni akitokea Liverpool, dili hilo likitajwa kugharimu Pauni milioni 46.
Licha ya mshahara mnono huo, bado Nunez hafiki kwa staa wa Manchester City, Erling Haaland, ambaye ndiye kinara wa mishahara Ligi Kuu ya England.
Haaland anakinga Pauni milioni 27 kwa mwaka, sawa na Pauni 525,000 kila wiki pale Etihad.
Mshambuliaji wa Liverpool raia wa Misri, Mohamed Salah, anashika nafasi ya pili kwa mshahara wake wa Pauni milioni 20, akifutiwa na Carlos Casimiro na Virgil van Dijk.
Nunez anayeondoka Anfield akiwa amezipasia nyavu mara 40 katika mechi 143, anakuwa mchezaji wa pili mkubwa kuipa kisogo Liverpool baada ya Luis Diaz aliyetimkia Bayern Munich.
Published:


