LAGOS, Nigeria
KOCHA wa timu ya soka ya wanawake ya Nigeria (Super Falcons), Justine Madugu, ameandika historia baada ya kuingia kwenye kinyang’anyiro cha tuzo za Ballon d’Or za mwaka huu.
Madugu aliiongoza Super Falcons kutwaa taji la fainali za Mataifa ya Afrika kwa soka la Wanawake (WAFCON) zilizofanyika mwaka jana huko Morocco.
Kutokana na kiwango bora cha timu yake, alitajwa kuwa ndiye Kocha Bora wa michuano hiyo.
Kwa sasa, Madugu anakuwa kocha wa kwanza raia wa Nigeria kuwania Ballon d’Or tangu tuzo hizo zilipoanzishwa mwaka 1956.
Published:


