10.7 C
New York

Partey aibukia La Liga

Published:

LONDON, Uingereza
BAADA ya kuachana na Arsenal, kiungo wa kimataifa wa Ghana, Thomas Partey, amemalizana na Villarreal ya Ligi Kuu ya Hispania (La Liga).
Partey aliyewahi kuwika La Liga akiwa na Atletico Madrid, alitamani kubaki Arsenal lakini mabosi wa klabu hiyo waligoma kumpa mkataba mpya.
Kiungo huyo anaondoka Emirates akiwa ameitumikia Arsenal kwa miaka mitano. Mkataba wake na Washika Bunduki hao wa London ulifikia ukomo mwishoni mwa Juni, mwaka huu.
Ripoti zinaeleza kuwa Partey mwenye umri wa miaka 32 amekubali mkataba wa miaka miwili na Villarreal.
Nyota wengine wanaoweza kuondoka Emirates majira haya ya kiangazi ni Oleksandr Zinchenko, Fabio Vieira, Albert Sambi Lokonga, Reiss Nelson na Leandro Trossard.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img