KWA saa 24 zilizopita, mashambulizi ya Israel katika Ukanda wa Gaza yamesababisha vifo vya Wapalestina 81, huku zaidi ya 800 wakijeruhiwa.
Asubuhi ya leo (Jumamosi), shambulizi la anga lilielekezwa katika Shule ya Jaffa, ambako mamia ya watu wa Gaza walikuwa wameweka makazi. Aidha, katika shambulizi jingine, watu 11, wakiwamo watoto, walipoteza maisha, kwa mujibu wa wafanyakazi wa Hospitali ya Al-Shifa.
Mmoja ya mashuhuda, Mohammed Haboub, aliliambia Shirika la Habari la Reuters kwamba alipoteza mpwa, baba na watoto wake katika shambulizi hilo. “Hakuna tulichowafanyia, kwanini wanatuumiza? Tumewahi kuwadhuru? Sisi ni raia tusio na hatia,” amesema Haboub.


