Na Mwandishi Wetu, Gazetini
Ripoti ya mwaka 2019 iliyotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto(UNICEF) Tanzania, zinaonyesha kuwa watoto Milioni 1.1 wenye umri wa miaka 0-17 ni yatima waliotokana na janga la UKIMWI.
Aidha, UNICEF imeeleza kuwa watoto wengine 6,500 wenye umri wa chini ya miaka 15 walifariki dunia kutokana na UKIMWI mwaka 2016.
Sambamba na hayo Ripoti hiyo iliyopewa jina la Tanzania Tunayoitaka Ajenda ya Watoto na Vijana ambayo imeenda sambamba na maadhimisho ya miaka 30 ya Mkataba wa haki za mtoto wa Umoja wa Mataifa inaonyesha kuwa kuna maambukizi mapya 10,000 kwa watoto chini ya miaka 14.