1.4 C
New York

Visual| Reli bado ina umuhimu

Published:

Treni au Garimoshi ni aina ya usafiri ambao umekuwapo miaka na miaka. Historia ya treni inahusu miaka mia mbili iliyopita ya ustaarabu wa kibinadamu wa kisasa, wakati ugunduzi huo mzuri ulipotumika kuleta mabadiliko katika tasnia, kuathiri kuenea kwa ubinadamu na njia tunayosafiri.

Tangu treni ya kwanza iliyosafiri kwenye reli za Uingereza ya viwandani mwanzoni mwa miaka ya 1800, treni zimesaidia watu kukuza ustaarabu, uchumi na faida nyingine lukuki. 

Aidha, historia inatukumbusha kuwa treni ya kwanza kabisa ulimwenguni ilionekana mnamo mwaka 1804. Treni hiyo iliweza kusafirisha tani 25 za vifaa vya chuma na watu 70 kwa umbali wa maili 10 (kilomita 16), katika historia yote, treni zimekuwa zikitumia mvuke, umeme, na dizeli (ingawa moja ya treni za mwanzo huko Merika zilikuwa na nguvu za farasi). Hivi sasa treni inakadiriwa kubeba karibu 40% ya shehena ya ulimwengu.

Mchango huo wa treni ambao hutumia reli, umeonekana bado una nafasi kubwa nchini Tanzania, kwani pamoja na ujio wa teknolojia mbalimbali ikiwamo kuimarishwa kwa miundombinu ya barabara sanjari na usafiri wa anga, lakini bado reli inatumiwa kusafirisha abiria na bidhaa mbalimbali ndani na nje ya nchi.

Hii ni sawa na kusema kwamba bado ujio wa mabasi ya kisasa sambamba na huduma ya ndege havijafanikiwa kuufuta kwenye ramani usafiri huu maarufu zaidi.

Wapo wanaoamini kwamba usafiri huo umekuwa ni nadra kupata ajali ikilinganishwa na njia nyingine zinazotumika kusafirisha abiria na mizigo ikiwamo kuimarika kwa miundombinu ya barabara na usafiri wa anga.

Umuhimu wa treni nchini Tanzania unadhihirishwa na takwimu ambazo zinaonyesha kuwapo kwa abiria ambao bado wanatumia usafiri huo kusafiri ndani ya nchi katika mikoa maarufu kama Tabora, Kigoma, Tanga na Mwanza kupitia reli ya Shirika la Reli Tanzania (TRC). Aidha, nje ya nchi kuna abiria wanaotumia usafiri huo kwenda nchi kama Zambia kupitia reli ya TAZARA.

MwakaAbiri wa TRCAbiri wa TAZARA
2006324,922298,092
2007315,507349,712
2008321,352344,135
2009374,121285,782
2010150,645303,203
2011328,508300,219
2012290,000288,140
2013333,45884,000
2014205,180202,000
2015296,816129,473
2016353,245151,687
2017386,442229,200
2018412,927201,400
2019368,403225,341

Aidha, mbali na abiria hao waliosafiri kwa njia ya reli, pia kuna tani za mizigo ambazo zilisafishwa kwa njia ya reli kwenda ndani na nje ya nchi kuanzia mwaka 2006 hadi 2019.

MwakaMizigo Tani(000)
20061,534,835
2007946,485
20081,304,020
2009993,587
2010963,103
20111,077,889
2012627,685
2013403,738
2014439,242
2015334,000
2016360,473
2017609,555
2018715,302
2019601,503

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img