21 C
New York

Olimpiki 2021; Nani kuivua ubingwa Brazil?

Published:

TOKYO, JAPAN

HUKU zikisikiliziwa ligi kubwa tano za Ulaya, mashabiki wa soka ulimwenguni watazitumia wiki chache za hivi karibuni kujipoza na michuano ya Olimpiki itayoanza kurindima kesho jijini Tokyo, Japan.

Jumla ya timu 16 ziko zimeshawasili Japan, tayari kwa mashindano hayo yanayotishiwa na uwepo wa janga la Corona.

Ikumbukwe, Brazil ni bingwa mtetezi baada ya kutwaa medali ya dhahabu mwaka 2016, michuano iliyoandaliwa nchini kwao.

Kundi la kifo liko wapi? Kundi A: Japan, Mexico, Ufaransa, Afrika Kusini. Kundi B: Honduras, Korea Kusini, New Zealand, Romania. Kundi C: Argentina, Australia, Misri, Hispania. Kundi D: Brazil, Ujerumani, Ivory Coast, Saudi Arabia.

Mfumo ukoje? Katika timu 16, yamapatikana makundi manne. Nane zitaishia hapo, na zilizobaki zitakwenda hatua inayofuata (robo fainali).

Ikimaanisha, kila kundi linatoa nafasi kwa timu mbili tu za juu kusonga mbele.00

Ufunguzi (kesho, Julai 22) ratiba ikoje?

Misri v Hispania Mexico v Ufaransa New Zealand v Korea Kusini Ivory Coast v Saudi Arabia Argentina v Australia – 11:30 BST Honduras v Romania – 12:00 BST Japan v Afrika Kusini Brazil v Ujerumani

Mechi zinachezwa wapi?

Kuna miji sita itakayotumika kwa mechi za soka la wanaume. Miji hiyo ni Kashima, Rifu, Saitama, Sapporo, Tokyo, na Yokohama. Hili ni chaka la mastaa EPL? Ndiyo, kwa mashabiki wa Ligi Kuu ya England (EPL), Olimpiki si ya kukosa kwani watawashuhudia mastaa wa klabu zao wakifanya yao nchini Japan.

Kwa jicho la haraka, unaiona Brazil ikiwa imekwenda Olimpiki ikiwa na beki wa Arsenal, Gabriel Martinelli, wakati Ivory Coast wao wanajivunia uwepo wa mastaa wa Manchester United, Eric Bailly na Amad Diallo.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img