9 C
New York

Ally Kamwe akiri kuvutiwa na TshabalalaNa Mwandishi Wetu

Published:

Na Mwandishi Wetu

Ofisa Habari wa klabu  ya Yanga Ally  Kamwe amesema licha ya kuwa yupo upande mwingine lakini ni shabiki mkubwa wa wachezaji  wa Simba, Mohammed Hussein ‘Tshabalala na Shomari Kapombe kutokana na  uwezo mkubwa wa nyota hao.

Kamwe ametoa kauli hiyo kipindi ambacho kuna na tetesi kuwa Yanga wanaitaka saini ya Tshabalala katika kuimarisha kikosi chao.

“Nchi hii hapa  hakuna mwanadamu anaweza akadharau uwezo wa Mohamed Hussein Zimbwe na Shomari Kapombe, Mimi mwenyewe ni shabiki mkubwa wa hao watu wawili ni wachezaji wazuri,” amesema Kamwe.

Hata hivyo Kamwe hajaweka wazi kuwa klabu hiyo inamhitaji mchezaji huyo baada ya kusema bado hawajaanza usajili wala kutoa orodha ya wachezaji wanaoondoka klabuni hapo.

“Kuanzia tarehe 20 mwezi huu ndiyo Yanga tutaanza kutoa taarifa rasmi ya nani katoka nani kaingia, sisi hatuna mambo ya ‘Thank You’ kipindi hiki,” amesema.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img