9 C
New York

Fountain Gate FC yabaki Ligi Kuu

Published:

Na Mwandishi Wetu

Klabu ya Fountain Gate  imefanikiwa kusalia kwenye Ligi Kuu  Tanzania Bara kwa msimu ujao baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Stand United katika mchezo wa mtoano uliopigwa kwenye Uwanja wa Tanzanite Kwaraa, mkoani Manyara.

Fountain Gate meshinda jumla ya mabao 5-1 katika michezo miwili ya mtoano  ya nyumbani na ugenini baada ya kushinda 3-1 katika mchezo wa kwanza uliochezwa kwenye Uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga na leo wakahitimisha kwa ushindi wa 2-0 nyumbani.

Mabao ya leo yamefungwa na Elie Mkono dakika ya 51 na Edger William dakika ya 90, hivyo kuihakikishia timu hiyo nafasi ya kuendelea kusalia  kwa msimu wa 2025/2026.

Ushindi huo umeleta furaha kwa mashabiki wa  timu hiyo kutokana na  kukwepa kushuka daraja kupitia  hatua ya mtoano.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img