13.1 C
New York

Bondia Debora apania kulipa kisasi

Published:

Na Mwandishi Wetu, Gazetini

Bondia  wa ngumi za kulipwa nchini, Debora Mwenda, ametangaza vita dhidi ya mpinzani wake Asia Meshack , akiahidi kulipa kisasi katika pambano la Dar Boxing Derby litakalofanyika Julai 26, 2025, jijini Dar es Salaam.

Amesema  pambano lililopita baada ya kupoteza alipata hasira kali hadi kulia ulingoni, hivyo bado ana machungu na hasira zote atazimaliza  mchezo ujao watakapokutana  tena na mpinzani wake.

Nimuambie tu mpinzani wangu Asia kuwa bado nina hasira  ya mechi niliopoteza mbele yake na  nililia.  Namuambia ajipange maana hiyo hasira ya kulia itakuja kumuishia yeye,” ametamba Debora.

Amesema mashabiki wake watarajie kuona mabadiliko ulingoni kwa kuwa amejipanga kuwapa burudani na kuondoka na ushini siku hiyo.

Hata hivyo amekiri kuwa mpinzani wake ni mzuri lakini amejiandaa vizuri kuhakikisha hawezi kurudia makosa yaliyomfanya apoteze pambano lilipita.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img