15.9 C
New York

Bunge lapitisha Bajeti ya Trilioni 2.44 wizara ya elimu

Published:

Na Ramadhan Hassan, Gazetini- Dodoma

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepitisha bajeti ya Sh Trilioni 2.44 kwa mwaka wa fedha 2025/2026 kwa ajili ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, huku Serikali ikiahidi kuongeza miundombinu na idadi ya walimu nchini.

Akihitimisha mjadala wa bajeti hiyo leo Mei 13, 2025, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, amesema Serikali kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais – TAMISEMI imejipanga kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia kwa kuongeza madarasa, vifaa vya kujifunzia pamoja na kuajiri walimu wapya.

“Tutaendelea kushirikiana na TAMISEMI kuhakikisha tunaboresha miundombinu ya shule na kuwepo kwa walimu wa kutosha katika maeneo yote ya nchi,” amesema Waziri huyo wakati wa kuhitimisha hoja za wabunge.

Bajeti hiyo imeungwa mkono na wabunge wengi waliopongeza hatua ya Serikali kuwekeza zaidi katika sekta ya elimu, lakini wakaitaka pia kuhakikisha usimamizi mzuri wa rasilimali, ili kuboresha ubora wa elimu hasa katika shule za msingi na sekondari.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img