6.7 C
New York

Visual: Elimu bado inahitajika kudhibiti TB nchini

Published:

Na Faraja Masinde, Gazetini

Licha ya kazi kubwa inayofanywa na Serikali katika kudhibiti Kifua Kikuu(TB) nchini ikiwamo kutoa matibabu bure lakini bado takwimu zinaonyesha kwamba ugonjwa huo umeendelea kuwasumbua wananchi walio wengi hapa nchini.

Katika kipindi cha miaka mitano mfululizo kuanzia 2018 hadi 2022, Mkoa wa Dar es Salaam umeendelea kurekodi takwimu za kuongezeka kwa watu wanaogundulika kuwa na chembechembe za ugonjwa huo.

Mathalani takwimu za mwaka 2018 zinaonyesha kuwa Mkoa wa Dar es Salaam ulikuwa na watu 15,481 waliobainika kuwa na vimelea vya TB kiwango hicho kinaonyesha kuongezeka mwaka 2022 na kufikia watu 16,659.

Wakati takwimu za Mkoa wa Dar es Salaam zikionyesha hivyo, upande wa zile za Jiji la Dar es Salaam zinaonyesha kuwa mwaka 2018 kulikuwa na watu 5,152 waliobainika kuwa na vimelea vya TB huku idadi hiyo ikiongezeka mwaka 2022 na kufikia watu 5,414.

Hii ni sawa na kusema kwamba bado kuna kazi kubwa ya kufanya ikiwa ni pamoja na wananchi kujitokeza katika vituo vya kutolea huduma za afya kwa ajili ya kufanya uchunguzi iwapo wana TB au la.

Ikumbukwe kuwa Takwimu za mwaka 2022 zinaonesha kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi 30 duniani zenye wagonjwa wengi wa TB ambazo uchangia 87% ya wagonjwa wote duniani (WHO 2021 ripoti).

Mwaka 2021 iilikadiriwa kuwa watu 132,000 waliougua TB hii ikiwa ni sawa na wastani wa uwiano wa wagonjwa 208/100,000.

Aidha, wagonjwa 87,415 waligunduliwa na kuwekwa kwenye matibabu mwaka 2021, watu 44,585 sawa na 35% hawakubainika na kuwekwa kwenye matibabu hivyo  kuendelea kuambukiza watu wengine katika jamii.

Hivyo ni jukumu letu kuendelea kuwatafuata na kuwaweka kwenye matibabu ili kupunguza maambukizi ya kifua kikuu katika jamii zetu na kutokomeza ugonjwa huo nchini. Vituo vyote vya huduma za afya nchini vinatoa huduma za TB na Ukoma kwa viwango tofauti kulingana na ukubwa na uwezo wa kituo.

Zaidi angalia usanifu wetu hapo juu.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img