MADRID, Hispania
KIUNGO wa Real Madrid raia wa England, Jude Bellingham, amesema tuzo ya Ballon d’Or haina maana yoyote kwake.
Kama hiyo haitoshi, nyota huyo wa zamani wa Borussia Dortmund amesema hajali kuhusu tuzo hiyo kwani ni ya waandishi wa habari.
Na badala yake, Bellingham amedai kuwa kwa sasa akili yake iko kwenye mapambano ya kuiwezesha Madrid kutwaa mataji chini ya kocha Jose Mourinho.
Bellingham ameibuka na madai hayo baada ya kuiongoza Madrid kupata ushindi dhidi ya PSV katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya uliochezwa jana Novemba 24, 2026.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 23, alishika nafasi ya 11 katika kinyang’anyiro cha tuzo hiyo kwa mwaka 2026.
“Ballon d’Or? Sijali. Hiyo ni kwa ajili ya waandishi wa habari, siyo mimi,” amesema Bellingham katika mahojiano yake na mwandishi wa Italia, Fabrizio Romano.


