16.6 C
New York

Muhaj Cup 2026 yafikia patamu, nusu fainali hii hapa

Published:

Na Editha William, Gazetin – KAGERA

RAUNDI ya kwanza ya mashindano ya soka ya Muhaj Cup imefikia tamati na sasa inasubiriwa hatua ya nusu fainali inayotarajiwa kuanza kuchezwa Novemba 24, 2026.

Kwa msimamo ulivyo baada ya kila timu kushuka dimbani mara tatu, Kashabo FC wanaongoza wakiwa na pointi tano baada ya ushindi wa mechi moja na sare mbili.

Fanicha wako nafasi ya pili kwa tofauti ya pointi mbili, wakiwa wametoa sare mechi zote tatu walizocheza, kama ilivyo Okmkisheyi iliyo nyuma yao kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.

Aidha, Mchikichini wako mkiani katika nafasi ya nne kwani wao wana sare mbili na kufungwa mechi moja, hivyo kukusanya pointi tatu.

Kwa mujibu wa mfumo wa mashindano, timu iliyomaliza nafasi ya kwanza [Kashabo FC] itakutana na iliyomaliza nafasi ya tatu [Omkisheyi FC], wakati ya pili [Fanicha FC] itavana na ya nne [Mchikichini].

Related articles

Recent articles