LONDON, Uingereza
MABINGWA watetezi, Arsenal, wamelazimishwa sare ya mabao 2-2 na Newcastle United katika mchezo wa leo Novemba 21, 2026, kwenye Uwanja wa St James’ Park.
Katika mchezo huo, Arsenal walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Eberechi Eze [Dk. 33], kisha Newcastle United wakasawazisha kupitia Harvey Barnes [Dk. 49].
Katika dakika ya 62 ya mchezo, wenyeji Newcastle United waliingia tena kwenye nyavu za Washika Bunduki, safari hii mfungaji akiwa ni Malick Thiaw.
Wakati Newcastle United wakiamini wameshatia mkononi pointi tatu, Noni Madueke aliwanyanyua vitini mashabiki wa Arsenal kwa bao lake la dakika ya 78, hivyo timu hizo kutoka sare ya mabao 2-2.
Kwa matokeo hayo, Arsenal wameendelea kubaki kileleni mwa msimamo wa Ligi kwa tofauti ya pointi sita dhidi ya Manchester City na Brighton, huku Newcastle wakiwa nafasi ya 12.


