21.2 C
New York

Cole kupewa mikoba Daraja la Pili

Published:

LONDON, Uingereza

MKONGWE wa Chelsea na Arsenal, Ashley Cole, ameingia kwenye mazungumzo na mabosi wa klabu ya Bromley inayoshiriki Ligi Daraja la Pili nchini Uingereza.

Timu hiyo inayoshika nafasi ya 22 kwenye Ligi hiyo, haina kocha mkuu kwa sasa baada ya kumfungashia virago Andy Woodman.

Cole alikuwa kocha kwa muda mfupi katika klabu ya Cesena ya Italia lakini alishinda mechi moja pekee kati ya nane alizokaa kwenye benchi.

Kwa nyakati tofauti, beki huyo wa kushoto wa zamani amewahi kufanya kazi na U-21 ya England, Pamoja na Chelsea, Everton na Birmingham City.

Akiwa huko Daraja la Pili, Cole atakutana na wachezaji wenzake wa zamani wa Arsenal, Jack Wilshere na Aaron Ramsey, ambao nao ni makocha.

Related articles

Recent articles