21.2 C
New York

Onana aingia rada za Waturuki

Published:

LONDON, Uingereza

KIPA wa Manchester United, Andre Onana, ameingia kwenye orodha ya wachezaji wanaowindwa na matajiri wa Galatasaray ya Uturuki.

Onana, raia wa Cameroon, kwa sasa anacheza kwa mkopo Trabzonspor ya huko Uturuki akitokea Man United.

Trabzonspor wanataka kumbakiza kipa huyo lakini changamoto inayowakabili ni dau kubwa waliloweka mezani mabosi wa Galatasaray.

Ripoti zinaeleza kuwa Trabzonspor wanamtaka Onana mwenye umri wa miaka 30 kwa ada ya Pauni milioni 8.38 lakini Galatasaray wamepanda dau zaidi.

Kwa upande wao, Man United bado hawajaonesha nia ya kumrudisha onana kikosini, hivyo kuipa Galatasaray nafasi kubwa ya kumsajili.

Related articles

Recent articles