MANCHESTER, Uingereza
BODI ya klabu ya Manchester United imekutana katika kikao ambacho kimejadili mustakabali wa timu hiyo chini ya kocha Michael Carrick.
Viongozi wa ngazi za juu klabuni hapo walitarajiwa kukaa mezani leo Oktoba 26, 2026, huku suala la hatima ya Carrick likiwa ajenda kuu.
Kikao hicho kimekuja baada ya Man United kutandikwa mabao 3-0 na Bournemouth katika mchezo wa jana wa Ligi Kuu.
Gazeti la Telegraph limeeleza kuwa Carrick yuko njiani kufungashiwa virago wakati huu timu hiyo ikiwa kwenye juu kidogo ya mstari wa kushuka daraja.
Ripoti zinaeleza kuwa majina ya makocha wakubwa kadhaa yameanza kuhusishwa na kibarua cha kiungo huyo wa zamani.
Miongoni mwa wanaohusishwa na kibarua chake ni Eddie Howe wa Newcastle United na kocha wa zamani wa timu ya soka ya Taifa ya Ujerumani, Julian Nagelsmann.


