15.3 C
New York

Pereira njiani kurudi mzigoni

Published:

LONDON, Uingereza

KOCHA asiye na kazi tangu alipofukuzwa na Nottingham Forest mwishoni mwa msimu uliopita [2025-26], Vitor Pereira, yuko njiani kurejea kazini.

Pereira, ambaye aliwahi pia kuinoa Wolves, aliajiriwa na Forest akichukua nafasi ya Sean Dyche lakini alidumu kwenye benchi kwa miezi michache tu kutokana na mwenendo mbaya wa timu hiyo.

Katika mechi zake 20, Forest ilishinda nane pekee, takwimu ambazo hazikuwafurahisha mabosi wa Forest na kuamua kumfuta kazi na kumuajiri Oliver Glasner.

Kwa sasa, kocha huyo raia wa Ureno amekuwa akihusishwa na Fulham ambayo ni kama imeanza kuchoka matokeo mabaya chini ya kocha Alvaro Arbeloa.

Wakati huo huo, Fulham pia inahusishwa na kocha asiye na kazi tangu alipofukuzwa na Tottenham, Thomas Frank.

Related articles

Recent articles