LONDON, Uingereza
SAINI ya winga wa Newcastle United, Bazoumana Toure, inawaniwa na klabu kubwa mbili za Ligi Kuu ya England [EPL], Arsenal na Manchester United.
Ni miezi michache tu imepita tangu Toure mwenye umri wa miaka 20 alipojiunga na Newcastle akitokea Hoffenheim ya Ujerumani kwa ada ya Pauni milioni 43.
Zipo taarifa zinazoeleza pia, kwamba Tottenham na Aston Villa nazo zimeonesha nia ya kumsajili mchezaji huyo.
Hata hivyo, hii si mara ya kwanza kwa Arsenal na Man United kuhusishwa na nyota huyo kwani ziliwahi pia kumfuatilia hata kabla ya kuondoka Hoffenheim.
Toure ameshafunga mabao mawili tangu aliposajiliwa na Newcastle, moja likiwa ni lile alilopachika dhidi ya Leeds United katika mechi ya EPL.


