23.8 C
New York

Nani kuvaa viatu vya Messi kikosi cha Argentina?

Published:

BUONES AIRES, Argentina

LIONEL Messi ameshastaafu kuitumikia timu ya soka ya Taifa ya Argentina na hivi karibuni alicheza mechi yake ya mwisho, ambapo waliifunga Benin mabao 2-0.

Messi [39], alifunga moja kwa mkwaju wa penalti na kufikisha mabao 126 katika mechi 208 alizocheza akiwa na ‘uzi’ wa Argentina.

Je, nani anakwenda kuwa shujaa mpya wa Argentina ‘La Albiceleste’ baada ya Messi kumaliza safari yake ya miaka 21?

Julian Alvarez (Atletico Madrid)

Kwa sasa, ndiye straika wa Argentina lakini haitoshangaza kuona akikabidhiwa jezi namba 10 aliyoiacha staa huyo. Martinez ana mabao 16 katika mechi 62 za timu ya taifa.

Alvarez hakuwa kwenye kiwango bora katika fainali za Kombe la Dunia zilizopita na msimu huu pia haujawa mzuri kwake kwani hajafunga bao katika klabu yake ya Atletico.

Nico Paz (Como)

Akiwa na umri wa miaka 22, Paz anayecheza Como ya Serie A amekuwa mchezaji muhimu kwenye kikosi cha Argentina.

Msimu huu, kiungo huyo wa zamani wa Real Madrid amefunga bao moja na ‘asisti’ tatu. Kwa timu ya taifa, ana mabao manne katika mechi 14 alizoitumikia Argentina.

Franco Mastantuono (Real Madrid)

Baada ya kupitia wakati mgumu akiwa Madrid, kinda huyo mwenye umri wa miaka 19 alihamia Fiorentina kwa mkopo hivi karibuni.

Katika Ligi ya Italia [Serie A], mshambuliaji huyo ameshafunga mabao matatu msimu huu. Hivi karibuni, alicheza mechi zote tatu za kalenda ya FIFA.

Alexis Mac Allister (Liverpool)

Kwa uzoefu alionao, haitoshangaza pia kuona jezi namba 10 ya Messi akikabidhiwa staa wa Liverpool, Mac Allister, ambaye ana mechi 57 za timu ya Taifa ya Argentina.

Katika mechi hizo, Mac Allister mwenye umri wa miaka 27 ameweza kufunga mabao saba na kutoa asisti saba. Amekuwa akitumia jezi namba 10 pia akiwa na klabu yake ya Liverpool.

Enzo Fernandez (Man City)

Ni nyota mwingine ambaye haitoshangaza kuona akikabidhiwa jezi ya Messi [namba 10]. Ni kiungo na umri wake ni miaka 25.

Enzo ameshacheza mechi 25, akifunga mabao nane na kutoa asisti sita. Hajawahi kuvaa jezi namba 10 katika maisha yake ya soka.

Related articles

Recent articles