23 C
New York

United, Spurs zagongana kwa straika

Published:

LONDON, Uingereza

KLABU za Manchester United, Tottenham na Everton zimejikuta kwenye ushindani mkali wa kuiwania saini ya straika wa Dinamo Zagreb, Dion Beljo.

Mtandao wa TEAMtalk umefichua kuwa klabu zote tatu zinasubiri usajili wa dirisha dogo la Januari, 2027, ili zipeleke ofa.

Beljo, raia wa Croatia mwenye umri wa miaka 24, ni moto wa kuotea mbali kwani amefunga mabao 12 katika mechi 14 zilizopita.

Kwa upamde wa mechi za Ligi Kuu ya Croatia, nyota huyo amefunga mabao 10 kwenye michezo saba tu ya hivi karibuni.

Wakati huo huo, klabu za Brentford, Newcastle United na Leeds United nazo zimeripotiwa kuingia kwenye mbio za kuisaka huduma ya mabao ya mchezaji huyo.

Related articles

Recent articles