15.3 C
New York

Nyuma ya pazia ziara za Rais Trump

Published:

WASHINGTON DC, Marekani

RAIS wa Marekani, Donald Trump, amefanya ziara 18 za nje ya nchi tangu aliporejea madarakani na Ulaya ndilo eneo alilotembelea zaidi [mara saba].

Ziara zake barani Ulaya imezigusa nchi za Vatican [Aprili 26, 2025], Ufaransa [Juni 15–17, 2026], Uholanzi [Juni 24–25, 2025], Uturuki [Julai 7–8, 2026], Scotland [Julai 25–29, 2025], Uingereza [Septemba 16–18, 2025], na Uswis [Januari 21–22, 2026].

Kama itakumbukwa, safari ya Vatican ilikuwa ziara yake ya kwanza ya nje ya nchi tangu aliporejea madarakani na alikwenda kwa ajili ya mazishi ya Papa Francis.

Kwa ziara ya Uingereza, akawa Rais wa kwanza katika historia ya Marekani kuitembelea mara mbili nchi hiyo akiwa madarakani. Ziara ya kwanza ni ile ya mwaka 2019.

Kwa upande mwingine, Rais Trump amefanya ziara nne katika Ukanda wa Mashariki ya Kati, akifika Saudi Arabia [Mei 13-14, 2025], Qatar [Mei 14–15, 2025], Umoja wa Falme za Kiarabu [Mei 15–16, 2025] na Israel [Oktoba 13, 2025].

Pia, kiongozi huyo amefika mara nne barani Asia, ambapo amekwenda Malaysia [Oktoba 26–27, 2025], Japan [Oktoba 27–29, 2025], Korea ya Kusini [Oktoba 29–30, 2025], na China [Mei 13–15, 2026].

Kwa Amerika ya Kaskazini, ambako ndiko iliko Marekani, Rais Trump ameitembelea nchi moja pekee, Canada, katika ziara yake ya Juni 15–16, 2025.

Barani Afrika, Rais Trump amefika mara moja pekee katika awamu yake ya pili madarakani, ikikumbukwa alivyoitembelea Misri [Oktoba 13, 2025].

Kufikia hatua hii ya muhula wake wa pili madarakani, Rais Trump hajafanya ziara katika nchi yoyote ya Amerika ya Kusini.

Related articles

Recent articles