MIAMI, Marekani
KUELEKEA robo fainali yao ya kesho dhidi ya Norway ya Erling Haaland, kambi ya timu ya soka ya Taifa ya England imetembelewa na mkongwe wao, David Beckham.
Nahodha huyo wa zamani wa England alifika kambini mjini Miami na kupokewa na wachezaji na viongozi wa kikosi hicho.
Presha ni kubwa mbele ya Norway iliyotinga robo fainali hiyo ya Kombe la Dunia kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Brazil.
Haaland ndiye aliyezamisha jahazi la Brazil kwa kufunga mabao yote mawili na kufikisha saba msimu huu wa Kombe la Dunia.
Kwa England, hii inakuwa mara yao ya 11 kufika robo fainali ya mashindano hayo. Imezidiwa na Brazil (15) na Ujerumani (14) tu kufika mara nyingi hatua hiyo.


