LONDON, Uingereza
KIUNGO wa pembeni wa Club Brugge ya Ubelgiji, Christos Tzolis, anataka kujiunga na Arsenal kupitia usajili wa majira haya ya kiangazi.
Mwandishi wa habari maarufu wa Italia, Fabrizio Romano, amesema winga huyo mwenye umri wa miaka 24 anasubiri kuona kama Leandro Trossard ataondoka Emirates ili aingie.
Mbelgiji mwenzake huyo anahusishwa na mpango wa kutimkia Uturuki anakowindwa na Besiktas.
Kwa upande wao, Arsenal wametajwa kuanza mazungumzo na wakala wa Tzolis ili kuona kama dili linaweza kukamilishwa haraka iwezekanavyo.
Tzolis amefunga mabao 43 kwa misimu miwili aliyoitumikia Club Brugge iliyomsajili mwaka 2024 akitokea Fortuna Dusseldorf ya Ujerumani.


