20.6 C
New York

Haaland naye hacheki, hachekeshi Kombe la Dunia

Published:

MEXICO CITY, Mexico

STRAIKA wa Manchester City, Erling Haaland, ameendeleza moto wake msimu huu wa Kombe la Dunia baada ya kufunga mara mbili katika ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Senegal.

Matokeo hayo yameiwezesha Norway kuvuka makundi na kuingia moja kwa moja katika hatua inayofuata ya 32 Bora.

Kwa mabao yake hayo, sasa Haaland amefikisha manne katika michezo miwili pekee waliyocheza.

Pia, anakuwa mchezaji wa sita katika historia ya Kombe la Dunia kufunga mabao mawili au zaidi baada ya mechi mbili za mwanzo.

Wakati huo huo, Haaland ameandika historia ya kuwa mfungaji bora wa muda wote wa timu yake ya Taifa, akiwa na mabao 59 katika mechi 52 alizocheza.

Kwa sasa, anamzidi mabao mawili mkongwe Kjetil Rekdal, ambaye ndiye aliyekuwa mfungaji bora wa muda wote wa Norway.

Aidha, dhidi ya Senegal imekuwa mechi ya 12 mfululizo kwa nyota huyo mwenye umri wa miaka 25 kuingia kambani.

Related articles

Recent articles