CAIRO, Misri
WINGA wa timu ya soka ya Taifa ya Misri, Mohamed Salah, ameeleza kufurahishwa na rekodi waliyoiweka msimu huu wa fainali za Kombe la Dunia.
Salah ameibuka baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya New Zealand katika mchezo wa alfajiri ya leo Juni 22, 2026.
Huo umekuwa ni ushindi wa kihistoria kwa Misri kwani ni wa kwanza kwa miaka yote ya ushiriki wao Kombe la Dunia.
“Ni jambo kubwa. Sijui niseme vipi. Ni mafanikio makubwa kwa wachezaji wote, wafanyakazi …” amesema Salah baada ya mechi hiyo.
Aidha, matokeo hayo yanaiacha Misri kileleni mwa Kundi G ikiwa na pointi nne, mbele ya Iran, Ubelgiji na New Zealand.
Kwa upande wake, Salah anaamini Misri inaweza kuandika historia mpya ya kuvuka hatua ya makundi kwa mara ya kwanza.


