LISBON, Ureno
LEJENDARI wa timu ya soka ya Taifa ya Ureno, Bruno Alves, amewasikia wanaoponda kiwango cha Cristiano Ronaldo msimu huu wa fainali za Kombe la Dunia.
Kwa mujibu wa Alves, wachezaji wakubwa kama Ronaldo hawana muda wa kuisha ubora na mchango wao ni mkubwa kikosini.
Kama hiyo haitoshi, ameeleza kuwa wakosoaji wa Ronaldo hawana kikubwa walichokifanya kwenye soka.
Amesisitiza kuwa wenye nafasi ya kumkosoa ni wale tu wenye mafanikio makubwa kuliko staa huyo wa Al Nassr.
“Tuheshimu wakongwe, hawana muda rasmi wa kuisha. Wengi wanakosa wakiwa hawana cha maana walichofanya kwenye soka,” amesema.


