CALIFORNIA, Marekani
WINGA wa kimataifa wa Hispania, Lamine Yamal, amempiku Lionel Messi katika orodha ya wachezaji wenye umri mdogo zaidi kufunga bao kwenye mechi ya kwanza ya Kombe la Dunia.
Yamal akiwa na miaka 18 na siku 323, alifunga moja katika ushindi wa mabao 4-0 walioupata Hispania mbele ya Saudi Arabia katika mchezo wa Kundi H.
Nyota wa zamani wa Brazil, Pele, ndiye kinda zaidi kufunga bao katika mechi ya kwanza ya Kombe la Dunia, akifanya hivyo alipokuwa na miaka 17 na siku 239.
Katika nafasi ya pili, ni Manuel Rosas, akifuatiwa na Gavi, Ibrahim Mbaye, Michael Owen, Nicolae Kovacs, na Dmitri Sychev.
Yamal anashika nafasi ya nane, akifuatiwa kwa karibu na Messi na Julian Green.


