19.5 C
New York

Aliyeitungua Ureno bado kidogo awe kipofu

Published:

HOUSTON, Marekani

URENO ya Cristiano Ronaldo ingeweza kuibuka na ushindi wa bao 1-0 katika mechi yao ya kwanza msimu huu wa Kombe la Dunia lakini haikuwa hivyo baada ya Yoane Wissa kuisawazishia DRC. Mechi ikamalizika kwa sare ya bao 1-1.

Pia, lilikuwa bao la kihistoria kwa DRC kwani haikuwahi kutikisa nyavu katika michuano ya Kombe la Dunia. Hii ni mara ya pili kwao kushiriki baada ya mwaka 1974.

Ni nani huyo Wissa anayekipiga Newscastle United? Unafahamu kuwa ni mchezaji aliyenusurika kupoteza uwezo wa kuona?

Miaka mitano iliyopita, Wissa akiwa Lorient ya Ligi Kuu ya Ufaransa (Ligue 1), alikuwa mahututi akiwa amelazwa katika moja ya hospitali nchini humo.

Ilikuwa Julai Mosi, 2025, ambapo mwanamke mmoja, Letitia P, aliingia nyumbani kwa Wissa kwa lengo la kumuiba binti yake.

Katika kutekeleza mpango wake, alipommwagia asidi, jambo lililosababisha mke wa Wissa kupiga simu ya dharura ili kupata msaada.

Baada ya kukamatwa na kufunguliwa mashitaka, bibiye huyo mwenye umri wa miaka 36 alikutwa na hatia na kuhukumiwa kifungo cha miaka 18 gerezani.

Wissa anasema tukio hilo lilimfanya kuwa mtu wa tofauti. “Tangu hapo, siwezi kukaa na watu nisiowajua. Sioneshi upendo kama zamani.

“Hata ninapotembea, naangalia nyuma mara kwa mara. Watoto wangu huwa wanauliza juu ya sura yangu, lakini ni wadogo sana kuwaambia.

Mwezi mmoja baada ya shambulio hilo, Wissa akiwa bado hajapona, aliondoka Ligue 1 na kujiunga na Brentford kwa mkataba wa miaka minne.

Related articles

Recent articles