20.9 C
New York

Scholes: Ronaldo wa sasa labda acheze kipa

Published:

MANCHESTER, Uingereza

KIUNGO wa zamani wa Manchester United, Paul Scholes, amesema Cristiano Ronaldo hastahili kuwa kiongozi wa safu ya ushambuliaji ya timu ya soka ya Taifa ya Ureno.

Ronaldo (41), alikumbana na ukosolewaji mkubwa baada ya Ureno kulazimishwa sare ya bao 1-1 na DRC katika mchezo wao wa kwanza msimu huu wa Kombe la Dunia.

Kabla ya michuano hiyo, Ureno ilikuwa ikipewa nafasi kubwa ya kufanya vizuri msimu huu, kama ilivyo kwa England, Hispania na Argentina.

Katika mechi ya kwanza, Ureno ilitangulia kwa bao la Joao Neves, kabla ya Yoane Wissa kuipatia DRC bao la kusawazisha.

Akizungumzia Ronaldo, Scholes amesema: “Akiwa na umri wa miaka 41, nafasi pekee anayoweza kucheza ni kipa tu, kwa upande wangu.”

Related articles

Recent articles