17.4 C
New York

Ancelotti afunguka kilichoiponza Brazil kwa Morocco

Published:

NEW YORK, Marekani

KOCHA wa timu ya soka ya Taifa ya Brazil, Carlo Ancelotti, amesema sare ya bao 1-1 waliyoipata mbele ya Morocco ilitokana na vijana wake kucheza vibaya kipindi cha kwanza.

Timu hizo zilikutana usiku wa kuamkia Juni 14, 2026 kwenye Uwanja wa wa New Jersey, Marekani, kila moja ikicheza mechi yake ya kwanza ya Kundi C msimu huu wa fainali za Kombe la Dunia.

Morocco walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Ismael Saibari (Dk. 21), kabla ya Vinicius Jr kuisawazishia Brazil (Dk. 32).

Akizungumza baada ya mchezo, Ancelotti amedai kuwa timu yake haikuwa bora kipindi cha kwanza, hasa kwa namna ilivyokuwa ikipoteza mipira.

“Nafikiri hii mechi, hasa kipindi cha kwanza, ilikuwa ngumu sana. Lakini nafikiri tulikuwa na hofu sana, tilipoteza mipira sana, na tulikosa balansi ndani ya uwanja,” amesema Ancelotti.

KITUO KINACHOFUATA

Brazil ‘Selecao’ watacheza mechi yao ya pili ya Kundi C ifikapo Jumamosi ya wiki ijayo, wakati Morocco ‘Simba wa Atlas’ wao watashuka dimbani siku moja kabla kwa mchezo wao dhidi ya Scotland.

Related articles

Recent articles