17.4 C
New York

Wenger aibuka na utabiri wake Kombe la Dunia 2026

Published:

PARIS, Ufaransa

KOCHA wa zamani wa Arsenal, Arsène Wenger, ameanza kwa kuitaja timu ya Taifa ya Ufaransa, akiipa nafasi katika zile anazoamini zitatwaa ubingwa wa Kombe la Dunia mwaka huu.

Katika mahojiano yake, Wenger ambaye kwa sasa ni mshahuri wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), amesema Ufaransa ina kikosi imara, pamoja na uzoefu wa kocha wake, Didier Deschamps.

“Tuna wachezaji wengi wa eneo la ushambuliaji … Unapocheza na Ufaransa, unafungwa muda wowote, hata zikiwa zimebaki dakika 20,” amesema.

Ufaransa ilitwaa ubingwa katika fainali za mwaka 2018 nchini Urusi lakini ilikosa taji msimu uliofuata (2022) baada ya kufungwa na Argentina katika mchezo wa mwisho.

Deschamps anatarajiwa kubwaga manyanga baada ya fainali za mwaka huu kumalizika, huku kiungo mwingine wa zamani wa timu hiyo, Zinedine Zidane, akipewa nafasi ya kurithi mikoba yake.

Related articles

Recent articles