LONDON, Uingereza
KUELEKEA fainali za Kombe la Dunia, yapo mengi ya kuvutia lakini kubwa ni kuona viungo wa kati (namba 8) wa viwango vya juu wakiwa sehemu ya michuano hiyo itakayoanza Juni 11, 2026.
Pedri wa Barcelona na timu ya Taifa ya Hispania atakwenda kwenye fainali hizo akiwa ndiye kiungo wa kati mwenye thamani kubwa zaidi kwenye soko la usajili (euro milioni 150).
Joao Neves wa PSG na Ureno anashika nafasi ya pili akiwa na thamani ya euro milioni 140, akifuatiwa na Declan Rice (Arsenal, England), euro milioni 120.
Katika nafasi ya nne ni Enzo (Chelsea) na Valverde (Real Madrid), ambao kila mmoja thamani yake sokoni ni euro milioni 90.
Wengine ni Zaire-Emery (PSG, euro milioni 80), Elliot Anderson (Forest, euro milioni 75), Mainoo (Man United, euro milioni 70), Mac Allister (Liverpool, euro milioni 70), na Guimaraes (Newcastle United, euro milioni 70).
WIinga wa thamani kubwa zaidi msimu huu wa Kombe la Dunia ni Lamine Yamal (Barcelona, euro milioni 200), wakati kiungo mshambuliaji ni Bellingham (Real Madrid, euro milioni 130).


