MILAN, Italia
MABINGWA mara nne wa Kombe la Dunia, timu ya taifa ya Italia, imeshindwa kufuzu fainali za mwaka huu zitakazofanyika Marekani, Canada na Mexico.
Hii ni zaidi ya nuksi kwa Italia kwani ni kwa mara ya tatu mfululizo mfululizo kwa wakali hao kuzikosa fainali hizo za FIFA.
Italia imekosoa tiketi baada ya kupoteza kwa penalti mchezo wao wa ‘play off’ dhidi ya Bosnia-Herzegovina.
Pio Esposito na Bryan Cristante walikosa mikwaju yao, hivyo Italia kupoteza kwa penalti 4-1, mchezo uliomalizika kwa sare ya bao 1-1 katika dakika za uwanjani.
Katika mchezo huo, beki wa Inter Milan, Alessandro Bastoni, hakumaliza dakika 90 baada ya kulimwa kadi nyekundu.
Kocha wa Italia, Gennaro Gattuso, anapaswa kumshukuru kipa wake, Gianluigi Donnarumma, ambaye aliokoa mabao tisa ya wazi.


