9.8 C
New York

Kombe la Dunia 2026; Kundi G

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini

KUMEKUCHA! Droo ya hatua ya makundi ya fainali za Kombe la Dunia ilichezeshwa nchini Marekani.
Kwa mara ya kwanza, fainali hizo zitashirikisha mataifa 48, huku mechi 104 zikitarajiwa kuchezwa katika viwanja mbalimbali vya Marekani, Mexico na Canada.

Tukijikumbushe; timu 42 zilishakata tiketi na sasa zinasubiriwa zingine sita zitakazopatikana kupitia mechi za ‘play-off’ zitakazochezwa Machi, mwakani.

Sasa, makala haya yanaliangazia Kundi G na kuchambua timu zilizopo kuelekea michuano hiyo itakayoanza Juni 11, mwakani.

Ni Kundi la Ubelgiji, Misri, Iran na New Zealand. Kwa upande wa Ubelgiji, wao hawakuwa na mwenendo mzuri katika mechi za kufuzu.

Chini ya kocha Rudi Garcia, timu hiyo ilifunga mabao nane na kuruhusu matano katika mechi hizo. Kiwango kibovu zaidi kiliwapa sare ya bao 1-1 dhidi ya Kazakhstan.

Misri, kwa upande wake, licha ya safu nzuri ya ushambuliaji ikiongozwa na Mohamed Salah na Omar Marmoush, mabeki nao walifanya kazi kubwa kuisaidia kufuzu.

Safu ya ulinzi iliruhusu mabao mawili pekee kwenye mechi 10 na Misri ilikata tiketi ikiwa haijaonja kichapo.
New Zealand wao walifuzu kibabe kwani walishinda mechi zote tano, pia wakifunga mabao 29, tisa kati ya hayo yakipachikwa na Chris Wood.

Iran, licha ya kwamba walifuzu wakiwa wamepoteza mechi moja pekee, hawatarajiwi kufanya makubwa katika fainali hizo. Ni kama ilivyo kwa New Zealand.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img