11.7 C
New York

Kilo 737 za mahindi yaliyopakwa rangi zakamatwa Kilimanjaro

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini-KILIMANJARO

JESHI la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro limekamata kilogramu 737 za mahindi ya kawaida yanayodaiwa kupakwa rangi na kufungashwa upya katika mifuko yenye majina ya kampuni zinazozalisha mbegu, kisha kuuzwa kwa wakulima kama mbegu za kupanda.

Katika operesheni hiyo iliyofanywa kwa kushirikiana na Kikosi Kazi (Task Force) na Taasisi ya Udhibiti wa Ubora wa Mbegu (TOSCI), pia vimekamatwa vifungashio 7,770, stika 260 zinazodaiwa kuwa bandia na lebo 3,000 zinazodaiwa kughushiwa.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Novemba 16, 2026, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, SACP Simon Maigwa, amesema operesheni hiyo imefanyika kufuatia malalamiko ya wakulima kutoka Halmashauri za Rombo, Moshi na Siha kuhusu kuuziwa mbegu zinazodaiwa kuwa zisizo na ubora.

Amesema uchunguzi uliofanyika uliwezesha kukamatwa kwa mtuhumiwa Mussa Jumanne Idowa, mkazi wa Moshi, Novemba 2, mwaka huu, kwa tuhuma za kujihusisha na utengenezaji na usambazaji wa mbegu zisizo na ubora ndani na nje ya mkoa huo.

Kwa mujibu wa Maigwa, uchunguzi wa awali umebaini kuwa mtuhumiwa huyo anadaiwa kununua mahindi ya kawaida, kuyapaka rangi na kuyafungasha katika mifuko yenye majina ya kampuni za mbegu zikiwemo SEEDCO, BAYER LIFE SCIENCE na CORTEVA AGRI-SCIENCE.

Related articles

Recent articles