MEXICO CITY, Mexico
MFANYABIASHARA maarufu wa dawa za kulevya nchini Mexico, Miguel Angel Felix Gallardo, amefariki akiwa na umri wa miaka 80.
Felix Gallardo ni miongoni mwa wanaotajwa kuwa na mtandao mkubwa wa dawa za kulevya katika nchi za Amerika ya Kusini, hasa Colombia na Mexico.
Akifahamika zaidi kwa jina la ‘Boss of Bosses’, Felix Gallardo alikuwa kiongozi wa genge la Guadalajara Cartel, ambalo lilikuwa tishio kwa uhalifu katika miaka ya 1980.
Kwa mujibu wa taarifa, amefariki akiwa hospitali, ikikumbukwa kuwa amekuwa akishikiliwa na vyombo vya dola tangu mwaka 1989.
Historia ya wauzaji wa dawa za kulevya duniani inamtaja kuwa ndiye anayefuata kwa ushawishi baada ya Pablo Escobar wa Colombia.
Zipo tafiti zinazoonesha kuwa Felix Gallardo alihusika katika asilimia 80 ya dawa zote za kulevya zilizokuwa zikiingia Marekani zikitokea.
Akiwa kwenye ukubwa wake, inaelezwa kuwa aliweza kuviweka mkononi vyombo vya dola na baadhi ya viongozi wa juu wa serikali za nchi zote za Amerika ya Kusini, hivyo kuwa na uhuru mkubwa wa kufanya biashara zake.


