Na mwandishi wetu, Gazetini – DAR
POLISI Kanda Maalum jijini Dar es Salaam inamshikilia mwendesha mtambo wa kuchimbia ardhi [excavator], Halidi Seleman kalaghe, kwa tuhuma za kuharibu mali za mwajiri wake.
Tukio hilo lilitokea jana Novemba 10, 2026, Mtaa wa Mvumoni Somangila, Kigamboni, Dar es Salaam, na kuzua taharuki baada ya video yake kusambaa mitandaoni.
Kalaghe [45], alichukau uamuzi wa kuiharibu mali baada ya kutokuelewa na mwajiri wake, ambaye ni Kampuni ya China Energy Engineering Group Guanxi Hydroelectric Construction Bureau CO. LTD inayofanya kazi za ujenzi wa barabara katika Manispaa ya Kigamboni.
Baada ya kile kilichoelezwa kuwa ni kutokuelewana na bosi wake, Kalaghe alichukua uamuzi wa kuingia kwenye mtambo na kuanza kuharibu mageti mawili na uzio wake, gari dogo lenye namba T 282 DEM aina ya Toyota Sienta.
Pia, akitumia mashine hiyo, aliharibu gari la kubeba mafuta namba T 391 EUN aina ya Sinortrack, ambalo ni mali ya kampuni, nyumba za muda zenye vyumba vitano na vyoo.
Wakati huo huo, polisi Dar es Salaam imemkamata mtuhumiwa Peter Mmasi [32], mkazi wa Kimara, kwa kosa la kumshambulia askari Sajenti Johnson Sylivery aliyekwua akimkamata kwa tuhuma za kutishia kumuua Carisma Amedeus Kileo.


