10.5 C
New York

Ndoa 200 zafungwa kwa pamoja Gaza

Published:

JERUSALEM, Palestina

LICHA ya kadhia kubwa wanayopitia raia wa Palestina katika Ukanda wa Gaza, ikiwamo kulala kwenye mahema, hawajaacha kutumia walau nyakati chache za furaha wanazopata.

Hii imethibitishwa na sherehe kubwa waliyofanya ya ndoa 200 kufungwa kwa pamoja katika eneo hilo linalosulubishwa na vita kati ya Israel na Kundi la Hamas.

Sherehe hiyo ya ndoa imeratibiwa na Shirika la Misaada ya Kibinadamu la Umoja wa Falme za Kiarabu [UAE], Operation Gallant Knight 3.

Israel imeendelea kutekeleza mashambulizi katika Ukanda wa Gaza, licha ya makubaliano ya kusitisha vita yaliyofikiwa Oktoba, 2025.

Vita hivyo viliamka upya Oktoba 7, 2023, baada ya Hamas kuripotiwa kuhusika katika shambulizi lililoua watu 1,200 na wengine 251 kutekwa nchini Israel.

Katika kujibu mashambulizi, Israel imeendesha operesheni nzito dhidi ya Hamas katika Ukanda wa Gaza na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 74,640.

Related articles

Recent articles