4.9 C
New York

Kenya: Watu 22 wafariki ajali ya basi na lori

Published:

NAIROBI, Kenya

WATU 22 wamefariki na wengine kadhaa kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha basi na lori kwenye barabara kuu ya Nairobi–Mombasa nchini Kenya, leo asubuhi.

Ajali hiyo imetokea majira ya saa moja asubuhi, wakati basi lililokuwa limebeba abiria waliokuwa wakirejea kutoka kwenye shughuli ya mazishi lilipogongana na lori.

Waliojeruhiwa wamekimbizwa katika Hospitali ya Kaunti Ndogo ya Mtito Andei, ambako wanaendelea kupata matibabu, huku miili ya waliofariki ikihifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali hiyo.

Kamishna wa Kaunti ya Makueni, Abdullahi Khalif, awali alithibitisha vifo vya watu 20, kabla ya idadi hiyo kuongezeka na kufikia 22.

Related articles

Recent articles