9.4 C
New York

Sudan Kusini kinara ukuaji wa uchumi Afrika

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini

SHIRIKA la Fedha la Kimataifa [IMF] limezitaja katika ripoti yake nchi 10 za Kusini mwa Jangwa la Sahara zenye kasi kubwa ya ukuaji wa uchumi kwa mwaka huu wa 2026.

Katika ripoti yake, IMF imeeleza kuwa uchumi katika eneo hilo la Kusini mwa Jangwa la Sahara umekuwa kwa asilimia 4.5, tofauti na matarajio ya awali ya asilimia 3.1.

Aidha, ripoti inafafanua kuwa Sudan ya Kusini imeongoza kwa uchumi wake kukua kwa asilimia 10.5, ikifuatiwa na Ethiopia [9.2%] na Rwanda [7.4].

Uchumi wa Ethiopia umepiga hatua kubwa hiyo kutokana na kuimarika kwa sekta ya kilimo na miundombinu, wakati Rwanda imeimarisha sekta ya huduma, ikiwamo utalii, na teknolojia.

Guinea na Benin nazo zimeonekana kupiga hatua ya ukuaji wa uchumi kwa asilimia 7.2 na 7.0. Uwekezaji katika uchimbaji wa chuma umeonekana kuinufaisha vilivyo Guinea.

Kama ilivyo Benin, Niger nayo ukuaji wa uchumi wake ni asilimia 7.0, mafanikio hayo yakichagizwa na mapato yatokanayo na biashara ya mafuta.

Uganda inafuata ikiwa na ukuaji wa uchumi wa asilimia 6.2, ikitegemea zaidi mafuta, kilimo cha kahawa na uchimbaji wa madini.

Tanzania na Ivory Coast zinafuata, kila moja ikiwa na ukuaji wa uchumi wa asilimia 6.0. Uchumi wa Tanzania unategemea zaidi utalii, usafirishaji wa dhahabu na sekta ya miundombinu. Ghana inakamilisha ‘Top 10’ ikiwa na ukuaji wa asilimia 5.7.

Related articles

Recent articles