18.3 C
New York

Urusi yashambulia daraja jingine Ukraine

Published:

KYIV, Ukraine

SHAMBULIZI la Urusi limeshambulia na kuharibu daraja kubwa la pili mjini Kyiv, ukiwa ni mwendelezo wa vita vya nchi hizo vilivyodumu kwa miaka minne.

Aliyethibitisha shambulizi hilo ni Meya wa Kyiv, Vitali Klitschko, ambaye pia ni lejendari wa mchezo wa ngumi za uzito wa juu duniani.

Akieleza zaidi, Klitschko amesema shambulizi hilo la asubuhi ya leo Oktoba 3, 2026, limelenga Daraja la Pivnichnyi la Kaskazini na kusababisha watu wawili kujeruhiwa.

Hivi karibuni, shambulizi la ndege zisizo na rubani la vikosi vya Urusi liliharibu Daraja la Pivdennyi la Kusini. Klitschko ameweka wazi kuwa kinachofanywa na maadui zao ni kuimaliza kabisa Kyiv.

Kwa upande wake, mamlaka za Urusi hazijaficha, na badala yake zimekiri kuhusika katika mashambulizi yote mawili. Urusi pia imewataka raia wa kigeni, wakiwamo wanadiplomasia, kuondoka mara moja mjini Kyiv.

Related articles

Recent articles