16.8 C
New York

Netanyahu alia na wapinzani

Published:

JERUSALEM, Israel

WAZIRI Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, amedai kuwa viongozi wa vyama vya upinzani wameanza kuungana kwa lengo la kumtoa madarakani. Uchaguzi Mkuu unatarajiwa kufanyika Oktoba 27, 2026.

Madai hayo ya Netanyahu yamekuja baada ya wanasiasa watano kukutana nyumbani kwa kiongozi wa Chama cha Yair Lapid, mjini Tel Aviv hivi karibuni.

Akizungumzia hilo, Netanyahu amedai kuwa kiongozi wa Chama cha Yashar, Gadi Eisenkot, anataka kuunda Serikali kwa kushirikiana na mwenzake wa Yair Lapid, Yair Golan.

Kwa upande mwingine, amesema pande mbili hizo zitaungana na Chama cha Bennett 2026, Yisrael Beiteinu, na wengine wa vyama vya Waarabu.

Hata hivyo, Netanyahu wa Chama cha Likud amesema anaamini wana ubavu wa kukabiliana na ushindani mkali kutoka kwa vyama hivyo.

“Ni Likud pekee itakayoweza kuvishinda,” amesema Netanyahu katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X [zamani Twitter].

Related articles

Recent articles