18.4 C
New York

Takwimu zinaongea: Brazil v Morocco

Published:

NEW YORK, Marekani

MECHI ya kwanza kwa timu hizo za Kundi C msimu huu wa fainali za Kombe la Dunia. Itachezwa usiku wa kuamkia kesho Julai 14, 2026, katika Uwanja wa MetLife, New Jersey, Marekani.

Brazil, mabingwa mara tano wa fainali hizo, dhidi ya Morocco, timu ya kwanza ya Afrika katika historia ya michuano hiyo kufika nusu fainali.

Hii itakuwa mechi ya nne kwa timu hizo kukutana. Katika michezo mitatu iliyopita, Brazil ilishinda miwili, huku Morocco ikiibuka na ushindi mara moja.

Mechi ya kwanza kati ya timu hizo ilichezwa Oktoba 9, 1997. Ilikuwa ya kirafiki iliyochezwa Brazil na wenyeji kushinda mabao 2-0.

Mwaka mmoja baadaye, Brazil na Morocco zilikutana hatua ya makundi kwenye Kombe la Dunia. Brazil ikaibuka na ushindi wa mabao 3-0.

Ronaldo alikuwa wa kwanza kuipatia bao Brazil, kabla ya Rivaldo na Bebeto nao kufunga na kuilazimisha kabisa jahazi la Morocco.

Mara ya mwisho ilikuwa mechi ya kirafiki iliyochezwa Marchi 25, 2023. Safari hii, Morocco walijitetea kwa ushindi wa mabao 2-1, licha ya kwamba ilikuwa ni mechi ya kirafiki.

Sofiane Boufal alifunga bao la utangulizi, kisha Casemiro akaisawazishia Brazil, kabla ya Morocco kumaliza kazi kwa bao la dakika ya 79 kupitia kwa Abdelhamid Sabiri.

Related articles

Recent articles