17.4 C
New York

Canada, Bosnia zamalizana kwa sare

Published:

TORONTO, Canada

HAKUNA mbabe. Ni dakika 90 za mchezo wa Kundi B uliochezwa Juni 12, 2026, ambapo wenyeji wa michuano ya mwaka huu ya Kombe la Dunia, Canada, wametoka sare ya bao 1-1 na Bosnia.

Bosnia walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 21 kupitia kwa Jovo Lukic aliyeunganisha kwa kichwa mpira wa kona, kabla ya Cyle Larin aliyetokea benchi kuisawazishia Canada (Dk. 79).

Aidha, Canada waliutwala mchezo huo kwa asilimia 60 dhidi ya 40, pia wakiongoza kwa pasi 390 dhidi ya 230 walizopiga wapinzani wao hao.

Pia, licha ya Canada kupiga mashuti 13, ni matatu pekee yaliyolenga lango. Bosnia walipiga nane na manne yakalenga lango la wapinzani la wapinzani wao.

Kituo kinachofuata

Baada ya mchezo huo wa kwanza, Bosnia watasubiri hadi Juni 18, 2026 ili kuivaa Uswis, wakati Canada watacheza siku inayofuata dhidi ya Qatar.

Related articles

Recent articles